Tanzia : MKE WA KINGUNGE AFARIKI DUNIA MUMEWE AKIWA AMELAZWA HOSPITALI
Mke wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, Peras Kingunge amefariki dunia leo Alhamisi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mtoto wa Kingunge, Kinje Ngombale amethibitisha taarifa hizo na kwamba kifo cha mama yake kimetokea wakati baba yake pia ni mgonjwa.
"Ni kweli mama amefariki na baba amelala kwa sababu ndio kwanza ametoka chumba cha upasuaji aling'atwa na mbwa. Tutamwambia akiamka," amesema
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: