JAMBAZI AUAWA AKITAKA KUWAPIGA RISASI POLISI SHINYANGA MWAKA MPYA 2018
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Joseph Dogani (50) mkazi wa kata ya Ndala Mjini Shinyanga anayedaiwa kuwa ni jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi sehemu mbalimbali za mwili wake akidaiwa kutaka kuwapiga risasi askari polisi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Januari 2,2018,Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule amesema tukio hilo limetokea Januari 1,2018 saa 9:45 alasiri.
Amesema Joseph Dogani alifariki papo hapo baada ya kupigwa risasi na polisi baada ya marehemu kutaka kuwapiga risasi askari waliokuwa wanamfuatilia.
“Mtuhumiwa alikuwa akijihusisha na matukio mbalimbali ya mauaji,unyang’anyi wa kutumia silaha na uvunjaji ,alikuwa anatafutwa kuhusiana na tukio la kujeruhi na kumpora mlinzi silaha aina ya shortgun iliyopatikana baada ya kuuawa kwa jambazi mwenzake”,ameeleza Kamanda Haule.
Kamanda Haule amesema baada ya kupekuliwa alikuwa akiwa na bastola yenye risasi nne ndani ya magazine.
Na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: