DIWANI WA KATA YA TURWA AJIONDOA CHADEMA NA KUHAMIA CCM


Zakayo Chacha akitangaza kujivua Chadema leo - Picha kwa hisani ya Waitara Meng’anyi
Katikati ni Zakayo Chacha, kulia ni mwenyekiti UVCCM Wilaya ya Tarime, na kushoto, katibu wa CCM wilaya ya Tarime Hamis Mkaluka
Diwani wa kata ya Turwa  wilaya ya Tarime mkoani Mara na mjumbe wa kamati kuu ya Wilaya Chadema Zakayo Chacha Zakayo amebwaga manyanga na kukihama chama na kutimukia CCM.

Akizungumza  leo Januari 5,2018 na waandishi wa habari katika ukumbi wa Goldland Hotel Zakayo amesema kwa sasa haoni haja ya kuendelea kuwa kwenye chama ambacho hakuna dira.


Hata hivyo amewashukuru wananchi wake kumuunga mkono kipindi cha uongozi wake kwani umefanikiwa kupeleka maendeleo kwao ambayo ni tofauti na kipindi vingine vilivyopita huku akiwaomba kuendelea jumla ushirikiano katika kusukuma gurudumu mbele.
Na Waitara Meng’anyi

Post a Comment

0 Comments