AUAWA KWA KUCHINJWA NA MUME WAKE
Mkazi wa kijiji cha Kitagasembe Kata ya Gwitiryo Wilaya Tarime Mkoani Mara aliyefahamika kwa jina la Bhoke Mwita ameuawa kwa kukatwa shingo upande wa kulia kwa kitu chenye ncha kali na mumewe Mwita Mganya kwa kumkataza asiuze ardhi.
Kaimu kamanda wa polisi Tarime Rorya Obadia Jonas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa baada ya kutekeleza unyama huo alitokomea kusikojulikana na jeshi la polisi linafanya kila juhudi kuhakikisha linamtia nguvuni.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kitagasembe Gabriel Mnanka alisema chanzo mauaji hayo ni migogoro ya ardhi kati mtuhumiwa na marehemu baada ya marehemu kukataa mumewe asiuze ardhi ya familia ndipo aliamua kufanya unyama huo
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: