YANGA NA SIMBA KUKINUKISHA FEBRUARI MWAKANI


Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya klabu Afrika, Yanga na Simba watawajua wapinzani wao leo na karata yao kwanza watarusha Februari 9-11, 2018.

Kwa mujibu wa kalenda ya CAF inaonyesha mashindano hayo yataanza Februari 9 na kumalizika Novemba 11 mwakani.

Katika mashindano ya mwaka huu mechi zote zitachezwa mwishoni wa wiki hakuna mechi ya katikati ya wiki kama ilivyokuwa msimu uliopita ambako mechi zilicheza Jumatano na Jumanne.

Kwa mujibu wa kalenda hiyo ya CAF, Yanga na Simba zitaanza hatua ya awali kwa mechi ya kwanza kuchezwa kati ya Februari 9-11 na marudiano itakuwa Februari 16-18.

Endapo zitafanikiwa kufuzu kwa hatua ya pili mechi hizo zitachezwa kuanzia Machi 9-11 na marudiano itakuwa Machi 16-18.

Ratiba ya hatua ya makundi itapagwa Aprili na mechi za makundi zitachezwa Mei 4-6 na kusimama kupisha Kombe la Dunia na kurudi tena Julai 27-29.

LIGI YA MABINGWA AFRIKA:

Raundi ya kwanza‚ mechi ya kwanza – Februari 9-11

Raundi ya kwanza‚ mechi marudiano – Februari 16-18

Raundi ya pili‚ mechi kwanza – Machi 9-11

Raundi ya pili‚ marudiano – Machi 16-18

Mechi ya kwanza Makundi – Mei 4-6

Mechi ya pili Makundi – Julai 27-29

Mechi ya tatu Makundi – Agosti 10-12

Mechi ya nne Makundi - Agosti 24-26

Mechi ya tano Makundi – Agosti 31‚ Septemba 1-2

Mechi ya sita Makundi – Septemba 14-16

Robo fainali‚ mechi ya kwanza – Septemba 28-30

Robo fainali‚ mechi ya pili – October 5-7

Nusu fainali‚ mechi ya kwanza – Oktoba 19-21

Nusu fainali‚ mechi ya pili - Oktoba 26-28

Fainali‚ mechi ya kwanza – Novemba 2-4

Fainali‚ mechi ya pili – Novemba 

KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Raundi ya kwanza‚ mechi ya kwanza – Februari 9-11

Raundi ya kwanza‚ mechi ya pili – Februari 16-18

Raundi ya pili‚ mechi kwanza – Machi 9-11

Raundi ya pili‚ mechi pili – Machi 16-18

Raundi ya tatu‚ mechi kwanza – Aprili 6-8

Raundi ya tatu‚ mechi pili – Aprili 13-15

Mechi ya kwanza Makundi – Mei 4-6

Mechi ya pili Makundi – Julai 27-29

Mechi ya tatu Makundi – Agosti 10-12

Mechi ya nneMakundi - Agosti 24-26

Mechi ya tano Makundi – Agosti 31‚ Septemba 1-2

Mechi ya sita Makundi – Septemba 14-16

Robo fainali‚ mechi ya kwanza – Septemba 28-30

Robo fainali‚ mechi ya pili – Oktoba 5-7

Nusu fainali‚ mechi ya kwanza – Oktoba 19-21

Nusu fainali‚ mechi ya pili- Oktoba 26-28

Fainali‚ mechi ya kwanza – Novemba 23-25

Fainali‚ mechi ya pili – Novemba 30‚ Desemba 1-2

Post a Comment

0 Comments