KICHUYA AJA NA HABARI MPYA ...INABIDI WAJIPANGE

LIGI Kuu Bara inatarajiwa kuendelea tena wikiendi hii na timu shiriki zinapaswa zijipange kwelikweli kwani winga ghali zaidi nchini, Shiza Kichuya ametamba atakuja kivingine na kutisha zaidi katika ligi hiyo.

Kichuya anayeongoza kwa kuifungia Simba mabao mengi zaidi tangu msimu uliopita (17) alisema; “Simba tuna raha kukaa kileleni na bila shaka mashabiki wetu watakuwa wana furaha mtaani, hilo linawafanya wapinzani wetu, waumize akili namna ya kurejea kwa kishindo,” alisema.

Kichuya alisema hilo litaleta changamoto kwa wachezaji kutaka kuonyesha ufundi wao na ukubwa wa majina yao mbele ya mashabiki wa timu zao, kitu alichokiona kama kinaongeza umakini wa kazi zao.

“Mchezaji mwenye malengo lazima ajipange na kujiuliza alifanya nini wakati ligi inachezwa na sasa anapaswa kuwa na jipya gani la kusaidia kutimiza malengo yao timu.”

“Nataka Simba ichukue ubingwa, hilo linanifanya niendelee kupambana kuhakikisha ndoto inatimia na kuweka rekodi ya kukumbukwa na vizazi vijavyo,” alisema nyota huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar.

MWANASPOTI

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.