Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC), Nehemiah Mchechu amekanusha taarifa zilizosambaa mapema leo kuwa amekamatwa na TAKUKURU na kuhojiwa. Asema yupo kwenye msiba wa mama yake huko Ukonga.
-
Awali, zilisambaa taarifa zinazoeleza kuwa Mkurugenzi huyo aliyesimamishwa kazi jana kupisha uchunguzi, amekamatwa na TAKUKURU kwa mahojiano na angefikishwa mahakamani siku ya Jumanne kujibu mashtaka, taarifa ambazo si za kweli.
0 Comments