MWAMUZI ELLY SASSI, ALIYECHEZESHA MECHI YA SIMBA NA YANGA AMJIBU HAJI MANARA
Baada ya msemaji wa Simba Haji Manara jana kusema mwamuzi Elly Sassi aliwaonea kwenye mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Yanga Novemba 28 mwamuzi huyo amejitokeza na kusema Haji Manara amekosa cha kuwaeleza Wanasimba
Elly Sassi amesema Haji Manara anatakiwa kujua sheria za soka kwanza ndio aongee vinginevyo aende TFF akapate mafunzo ya kuwa mwamuzi sio kuangalia tukio moja kisha kulitafsiri kiushabiki.
“Nafikiri Haji Manara amekosa cha kuwaambia Wanasimba lakini matukio na maamuzi ya uwanjani siku ya mchezo hayana utata wowote kwa watu wanaojua sheria za soka ndio mana baada ya mchezo wakufunzi mbalimbali wa CAF walinipongeza”, amesema Elly Sassi.
Mwamuzi huyo ambaye amejizolea sifa miaka ya hivi karibuni kutokana na uchezeshaji wake ameenda mbali zaidi na kutafsiri kisheria matukio ambayo Manara anahisi yalipaswa kuwa penalti.
“Tukio la Yondani kisheria ni kweli alishika, lakini dhamira na namna ya tukio lilivyokuwa mkono haukuwa na mawasiliano na mpira na alikuwa ameruka juu katika harakati za kuokoa mpira ukafata mkono wala hakutumia mkono kuokoa mpira huo sawa na tukio la Tshishimbi”, amesema Saasi.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi