Makubwa!! WAMUOGESHA MFANYABIASHARA MWENZAO WAKIWA SOKONI

KULIKUWA na kizaazaa katika soko la Wakulima, Nakuru Kenya baada ya wachuuzi wa kike kumwosha kwa nguvu mwenzao wa umri wa makamo baada ya malalamishi kwamba alikuwa ananuka.

Wanawake hao walilalamika kuwa mwenzao huyo wa umri wa miaka 35 alikuwa amekaa siku nyingi bila kuoga.

Walisema hili lilikuwa likiwaharibia biashara kwa kuwafukuza wateja.

Inadaiwa walichukua hatua baada ya wachuuzi wa kiume kutisha kumwosha wenyewe iwapo wachuuzi hao wa kike wangekosa kufanya hivyo.

Walimfumania Jumatano asubuhi na kumwosha hadharani kisha wakamnunulia sabuni, taulo na beseni ili awe akitumia kuoga.

Bi Loise Gathoni na Miriam Kerubo, walioongea kwa niaba ya wachuuzi walisema harufu iliyotokana na kutooga kwa mwenzao ilikuwa imewakosesha biashara kwa wiki tatu.

Kisha hicho kilivutia umati mkubwa ambao ulishangilia huku wanawake wakiunda ‘ua wa binadamu’ kumzingira akioshwa kuhakikisha umma hauoni uchi wake.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.