Habari kutoka Wilayani
Hai ,mkoani Kilimanjaro watu watano wamepoteza maisha na wengine wanne
wakijeruhiwa baada ya lori kugongana uso kwa uso na Noah maeneo ya
kikavu kwa Sadala.
Daktari wa zamu hospitali ya wilaya ya Hai,Agness Temba amesema amepokea miili ya watu wa tano.
Amesema miili ya marehemu imehifadhiwa
katika hospitali ya wilaya ya Hai, na majeruhi wamekimbizwa katika
hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi.
0 Comments