
Baada ya taarifa kuenea kwenye mitandao ya kijaamii kwamba kocha wa Yanga George Lwandamina anakaribia kujiunga na kabu yake ya zamani Zesco United ya Zambia, afisa habari wa Yanga Dismas Ten amesema kocha huyo amekwenda Zambia kwa ajili ya matatizo ya msiba wa mpwa wake.
Ten amesema Lwandamina anatarajia kurejea nchini siku ya Jumatatu ijayo kwa ajili ya kuendelea na maandalizi kwa mechi za ligi zinazofuata.
"Taarifa pekee kutoka Yanga ni kwamba mwalimu amekwenda Zambia kwenye msiba na anarejea jumatatu, msiba ni jambo ambalo linamkuta kila mtu na huwezi kuliepuka na linapokufika huna budi kushiriki kwa yoyote ile".
Hilo la Zesco siwezi kuzungumza kwa sababu mimi sipo Zesco na kama inazungumzwa kwenye mitandao huwezi kuzuia watu kwenye mitandao ndio sehemu yao kuzungumza.”
"Lwandamina bado ni mwajiriwa wa Yanga ndio maana nimesema kwamba amekwenda Zambia kwenye msiba na atarejea Jumatatu kwa ajili ya matayarisho ya michezo inayofuata" alimaliza Dismas Ten.
0 Comments