Hatari sana!! MBUNGE MWINGINE APIGWA RISASI

MBUNGE wa Mathare, Anthony Oluoch, Jumapili alilazwa hospitalini baada ya kujeruhiwa katika hali tatanishi, katika mtaa wa Babadogo, jijini Nairobi, kwenye mkutano uliohutubiwa na kinara wa NASA Raila Odinga juzi.
Bw Oluoch alikimbizwa katika Nairobi Hospital akiwa na jeraha la mguu, ambapo NASA ilidai alipigwa risasi na polisi, huku baadhi ya ripoti zikisema kwamba alianguka kutoka kwa gari lake wakati wa mkutano huo.

Bw Odinga alikuwa amefika mtaani humo, baada ya madai kwamba watu kadhaa kutoka jamii fulani walikuwa wameuawa usiku wa kuamkia jana katika hali isiyoeleweka.

Hata hivyo, viongozi wa NASA waliomtembelea hospitalini walidai kwamba polisi walikuwa wamelenga kumuua, kwa kumpiga risasi, ila wakashindwa.

Na ingawa wanahabari hawakuruhusiwa kumwona mbunge huyo, Bw Odinga alilaani tukio hilo, akisema kwamba polisi sasa wameanza kuwageukia viongozi, baada ya kuwaua wananchi.

“Hii ni dalili ya mwanzo mbaya kwa taifa letu. Polisi wameanza kutumiwa na serikali kuwamaliza viongozi wa Upinzani,” akasema Raila, kwenye kikao na wanahabari hospitalini humo.

Hilo linajiri baada ya mbunge wa Kathiani, Robert Mbui (Wiper) kujeruhiwa baada ya makabiliano makali kuzuka kati ya polisi na wafuasi wa NASA, Ijumaa, wakati Bw Odinga alirejea nchini kutoka ziara ya siku 10 barani Ulaya.

Na kwenye taarifa jana, Wiper ilikashifu vikali shambulio hilo, ikisema mbunge huyo alilengwa kwa msimamo wake katika kupinga udhalimu wa utawala wa Jubilee.

“Hatutaogopa vitisho vyovyote dhidi yetu. Tutaendelea kutetea demokrasia, hadi pale uhuru kamili wa kujieleza utarejea nchini,” kikasema chama.

Kwa hayo, kilisema kuwa vitendo hivyo havitawatisha, ila vimewapa motisha zaidi katika kuendeleza nia yao ya “kuikomboa” nchi.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.