WACHEZAJI WA YANGA WAZIDI KUNEEMEKA....WAMWAGIWA MAPESA
Kundi linalojiita Yanga 4 Life ambalo limekuwa na Utaratibu wa kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri kwenye kila mechi inayohusisha YANGA limeendelea kutoa zawadi kwa wachezaji wa Yanga wanaofanya vizuri na siku ya jana jumaanne ya 31.10.2017 wachezaji Ibrahim Ajib, Papy Kabamba maarufu kama Tshishimbi na golikipa namba 1 wa timu hiyo Youthe Rostand wamekula pesa zao.
Kati ya wachezaji hao Ibrahim Ajib ndiye aliyekula mkwanja mrefu zaidi kiasi cha shilingi milioni 1 mara baada ya kuwa mchezaji bora katika michezo miwili ya kanda ya ziwa, mchezo kati ya Kagera Sugar na Yanga na ule kati ya Stand United na Yanga kila mchezo amepewa Laki 5 kama mchezaji bora wa Mechi.
Naye Mkongomani Papy Kabamba Tshishimbi amepewa zawadi ya laki 5 kama mchezaji bora wa mechi ya watani wa Jadi Simba na Yanga ikiwa ni mara yake ya pili kuzawadiwa kwenye mchezo wa watani wa jadi na Yanga 4 Life wa Kwanza ukiwa ni ule wa Ngao ya Jamii.
Naye Kipa Rostand Youthe amepewa zawadi ya Laki 2 pamoja na kilinda Ugoko na Viatu vya kuchezea Soka (Six).
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi