JULIO AWAPA ONYO KALI SIMBA
Hatimaye Jamhuri Kihwelu JULIO kocha wa Dodoma Fc na Mwanachama wa Klabu ya Simba amefunguka Kuhusu kocha Wa Simba Mcameron Joseph Omog.
Julio amewataka Simba kuacha Kumuingilia Omog katika Majukumu yake hali ambayo inamchanganya
Mimi nitoe tahadhari kwa timu yetu ya Simba kutokana na jinsi ilivyo, sisemi kama mwalimu Omog ni mbaya ila kuna watu wanamchanganya ilimradi aonekane hafai kwasababu kuna watu wanahisi Simba wanaijua na wanaweza kufanya mambo mazuri ambayo hayatusaidii matokeo yake kunakuwa na malumbano na mwalimu kutokuwa na haki ya Kufanya vizuri.
JULIO ambaye kwa vipindi tofauti amecheza Simba na kuwa Kocha wa timu hiyo pia amesema hakukuwa na haja ya kumfukuza MAYANJA kwa kipindi hiki cha katikati ya ligi,. Baadhi ya washabiki,wapenzi na wanachama wa Simba wamekuwa wakitaka kocha Omog afukuzwe Simba kwa sababu mbalimbali.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi