SIMBA SC YAKUMBWA NA BALAA KUBWA UWANJA WA UHURU

Simba imepanga kucheza na timu ya jeshi ya Hardrock ya Pemba leo jioni kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Ashanti nayo imepanga kuikabili Yanga leo kwenye uwanja huo huo . 

Dar es Salaam. Simba na Ashanti United zimeingia vitani kuwania Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuutumia katika mechi zao za kirafiki zitakazofanyia leo Jumapili.
Simba imepanga kucheza na timu ya jeshi ya Hardrock ya Pemba kesho jioni kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Ashanti nayo imepanga kuikabili Yanga kesho kwenye uwanja huo huo .

Awali Simba ilikuwa icheze na Hard Rock juzi Ijumaa  lakini ikapigwa stop na kuambiwa kuwa uwanja huo siku hiyo utatumika kwa ajili ya mazoezi ya Botswana ambayo ilikuwa ikijiandaa kucheza na Taifa Stars jana.
Afisa Habari wa Ashanti United, Adam Kinyogoli alisema wanachojua leo wao ndio wanatakiwa kuutumia uwanja huo kuikabili Yanga hivyo Simba wakatafute uwanja mwingine.

"Tulishaomba kucheza na Yanga Jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru hivyo hiyo mechi ya Simba hatuitambui kwani ninavyojua Simba ilitakiwa kuutumia uwanja huo Ijumaa(jana) lakini wanajua wenyewe sababu za kuhairisha hiyo mechi siku hiyo"alisema Kinyogoli

Alipoulizwa Kinyogoli kama endapo wataenda uwanjani na kukutana na Simba itakuaje?alijibu" Itajulikana uko uko kwani ninavyojua kuwa sisi ndio wenye haki ya kuutumia huo uwanja kesho sasa Simba wakija nao shauri yao".

Alipoulizwa tena je kama wamiliki wa Uwanja wakiwazuia kuutumia uwanja huo na kuiruhusu Simba iutumie watafanyaje, alijibu" Mpaka jioni hii hakuna taarifa zozote za kutuzuia kucheza mchezo huo na sidhani kama itatotea hilo".

Naye mkuu wa mawasiliano wa Simba,Haji Manara alisema anachojua ni kwamba leo wanacheza mchezo wa kirafiki kwenye Uwanja wa Uhuru hivyo hizo taarifa za mechi nyingie hawana.

"Sisi tunacheza mechi kesho na Hard Rock saa hizo taarifa za mechi ya Yanga na Ashanti sizijui"alisema Manara