HAJI MANARA AENDELEA KUMUANDAMA PAPY KABAMBA TSHISHIMBI

Wakati Ligi Kuu Bara imesimama kwa wiki moja kupisha mechi za Kimataifa, tambo, kejeli na utani umeamia kwenye mitandao ya kijamii

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara ameendelea kumuandama nyota mpya wa klabu ya Yanga raia wa Congo, Papy Kabamba Tshishimbi.
Papy Tshishimbi amejiunga na Wana jangwani akitokea klabu ya Mbabane Swallows inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Swaziland. 
Kupitia akaunti yake ya instagram, Haji Manara ameposti picha ya Tshishimbi na ya mwanamuziki wa Tanzania, Shilole, na kuambatanisha maneneo ya utani kwa nyota huyo wa Yanga kuwa iweje Mwanaume na Mwanamke wakafanana majina.

"Daah huyu Shilole vp?huyo ni mwanamme ww demu,vp mtumie jina moja?au ndo vile tena!!" ameandika hivyo msemaji huyo , Haji Manara