Mmiliki wa MALUNDE1 BLOG ambaye ni mwenyekiti wa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Kadama Malunde amekamatwa na jeshi la polisi alipokuwa akitekeleza majukumu yake kwenye tukio la Wananchi kufunga barabara mjini Shinyanga.
Tukio hilo limetokea asubuhi hii katika mtaa wa Magadula Ngokolo Manispaa ya Shinyanga ambapo wananchi waliamua kufunga barabara hiyo kutokana na kuchoshwa na vumbi kali linalotokea pindi magari yanapopita katika barabara hiyo.
Vumbi hilo kali linatokana na ujenzi wa muda mrefu wa barabara hiyo amabapo miezi sita iliyopita mkandarasi alichanganya mchanga na simenti na kumwaga katika barabara hiyo kasha kuitelekeza na hivyo kusababisha vumbi kali kupita kiasi linaloathiri shughuli na afya za wakazi wa eneo hilo