UHURU WA KUPATA HABARI NI SHIDA TANZANIA

Mkurugenzi wa Kituo cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB), Deus Kibamba amesema bado hakuna uhuru wa kupata taarifa nchini.

Akizungumza katika mkutano wa wadau wa habari kutoka Tanzania na Nigeria, Kibamba amesema ni lazima Serikali iandae kanuni itakayoiwezesha sheria ya haki ya kupata taarifa ambayo imesainiwa na Rais John Magufuli siku za karibuni kuanza kufanya kazi kabla ya kumalizika mwaka huu.

Amesema kiuhalisia hakuna uhuru wa kutoa maoni na kupata taarifa kama awali kiasi cha kuwafanya wanaharakati na wadau mbalimbali waliokuwa wakitoa maoni kuogopa kufanya hivyo.

Kibamba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba Tanzania, amefafanua kuwa ili sheria ya huduma ya vyombo vya habari ifanye kazi ipasavyo inatakiwa kwenda sambamba na sheria ya haki ya kupata taarifa