TUNDU LISSU AFUNGUKA BAADA YA KUTOKA RUMANDE

Tundu Lissu anasema baada ya kukamatwa na jeshi na polisi alizungushwa sana polisi na mwisho wa siku walimpeleka sehemu katika kituo cha afya ili apimwe mkojo lakini anadai alikata kupimwa mkojo kwani alikuwa anatuhumiwa kwa kosa la uchochezi lisilo husiana na kipimo cha mkojo.

"Nilizungushwa sana siku ile lakini mwisho wa siku nikapelekwa maeneo ya Ocean Road hospitali ya kansa nikaambiwa Mhe. tunahitaji tukupime mkojo wako, nikamwambia nyie askari mimi nimeshtakiwa kwa uchochezi hivyo kupima mkojo unathibitishaje uchochezi kwa kupima mkojo. Wakasema sisi kuna vitu tunavitafuta, nikawaambia kama kuna vitu mnatafuta wakanishtaki kwanza kwa hilo kosa ili sasa muende kwa hakimu mkamwambie kuwa mnawasiwasi na mimi kuna vitu mnavitafuta mnaweza kuvipata kwenye mkojo wangu, ila kama hajampata 'order' ya hakimu kwangu mkojo hamjapata" alisema Tundu Lissu 
Aidha Mhe Tundu Lissu anasema kuwa walikuwa wanafanya hivyo ili wapate vitu vya kuandikwa kwenye vyombo vya habari kwamba amepimwa mkojo ili waone kama kuna dalili za madawa ya kulevya na kusema ingewezekana Polisi wakasema kuwa yeye anaongea maneno mabaya kwa kuwa anatumia dawa ya kulevya.

Tundu Lissu aliendelea kulituhumu jeshi la Polisi kuwa wapo baadhi ya polisi wanatengeneza sana kesi na kuwabambikia watu kesi na kutengeneza ushahidi wa uongo
Hata hivyo Tundu Lissu amesema kuwa yeye mwenyewe hapendi kulala rumande na kuacha sehemu nzuri ya kulala yeye na familia yake, anadai kuwa hapendi kukamatwa na polisi wala kulala rumande wala magereza lakini kwenye masuala ya msingi yupo tayari kwa lolote lile.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.