ABDI BANDA ATEMBELEA KAMBI YA SIMBA NA KUAHIDI JAMBO HILI KUBWA

Beki wa Kimataifa kutoka nchini Tanzania Abdi Banda ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Baroka FC nchini Afrika Kusini leo ametembelea kikosi cha Simba katika kambi yake ya mazoezi nchini Humo.

Banda amejiunga na klabu ya Baroka FC akitokea katika klabu ya Simba, ambapo moja kati ya ahadi zake wakati anaondoka ni kama atapata nafasi ni lazima atajitahidi kufika kwenye Simba Day kwa ajili ya kutoa sapoti kwa wachezaji wenzake lakini pia kuungana na mashabiki wote wa Simba kwenye siku hii muhimu.