MCHUNGAJI WA KANISA AFARIKI BAADA YA KUGONGA DARAJA MAJARUBANI KAHAMA

Mchungaji wa kanisa la Divine mkazi wa Nyahanga mjini Kahama Beckam Gadson Joseph (24) amefariki dunia baada ya pikipiki yenye namba za usajili MC 446 AFP SANLG kugonga daraja na kupinduka katika eneo la Kiinza Majarubani wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACM Muliro Jumanne Muliro mchungaji huyo wa kanisa la Divine alikuwa anatokea Kiinza kwenda Kahama mjini ndipo akagonga daraja kisha kupinduka na kupoteza maisha.

Kamanda Muliro amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva huyo na mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya wilaya ya Kahama.