MASENGWA BLOG YATOA OFA KWA WANAMZIKI WOTE CHIPUKIZI

Katika suala zima la kuhakikisha vipawa vya vijana vinapaa juu na kujulikana ndani na nje ya Tanzania, MASENGWA BLOG imetoa ofa ya siku tatu (Ijumaa, jumamosi na Jumapili) tarehe 12-14/05/2017  kwa wanamziki wote walio wa Afrika mashariki kuwa itatangaza kazi zao bure kabisa ili kuinua vipawa vyao. Unachotakiwa kufanya, tuma wimbo wako mmoja ukiambatanisha na picha yako au kava la wimbo kwa njia ya whatsapp kwenda namba +255753336000.

Nyimbo hizo zitumwe siku ya Alhamis tarehe 11/05/2017 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni na baada ya hapo zoezi hilo litafungwa ili kupisha muda wa kuandaa nyimbo hizo zirushwe kwenye blog kuanzia siku ya Ijumaa hadi Jumapili.

NB: Msanii mmoja, wimbo mmoja tu.
MASENGWA BLOG IPO KWA AJILI!!!