LOWASSA AWALILIA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA BASI KARATU

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ametuma salamu za rambi rambi kutokana na tukio la watu 32 kufariki dunia katika ajali ya basi.

Waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea jana asubuhi Karatu, ni wanafunzi 29, walimu wawili, pamoja na dereva wa gari hilo.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali hiyo, ni ajali mbaya ambayo inaifanya siku hii kuwa mbaya katika historia ya nchi yetu,”alisema

Miongoni mwa wanafunzi waliofariki ni pamoja na wanaume 11 na wasichana 18.

Kadhalika maiti 32 zikiwamo za walimu wawili, dereva mmoja na wanafunzi 29 zilipokelewa katika Hospitali ya Lutheran Karatu.