BREAKING NEWS!! ASKOFU NKOLA WA KANISA LA AICT DAYOSISI YA SHINYANGA ATUMBULIWA

Kanisa la AICT nchini Tanzania limemstaafisha askofu mkuu wa kanisa hilo Dkt John Kanoni Nkola na kumtaka askofu mwingine wakanisa hilo John Bunango kujiuzula nafasi hiyo kutokana na matumizi mabaya ya fedha za kanisa.

Kanisa hilo pia limefukuza kazi ya uchungaji wachungaji watatu ambao ni Katibu mkuu wa kanisa hilo Mchungaji Jakobo Mapambano,mchungaji Dkt Meshack Kulwa.
na Mchungaji Emmanuel Isaya.
Hatua hiyo imechukuliwa siku chache tu baada ya Shule inayomilikiwa na kanisa hilo kupigwa mnada na kulisababishia kanisa hilo hasara.

Tangazo la kanisa kuchukua hatua hizo limetangazwa muda huu katika kanisa la AICT Kambarage na Askofu mkuu wa kanisa la AICT nchini Tanzania Askofu Silasi Kezakubi (pichani) kutokana na maamuzi ya baraza la utendaji la sinodi kuu AICT.


Taarifa kamili tutawaletea hivi punde hapa MASENGWA BLOG

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.