MADHARA YA KULA NYAMA NYEKUNDU

Watu wengi tunapenda sana kula nyama,  hilo halina ubishi, kama yupo ambaye hapendi nyama basi anyooshe kidole. Lakini licha ya kupenda nyama je wajua ulaji wa nyama kwa wingi una athari kiafya? Usishangae huo ndio ukweli.
Kwani madaktari bingwa wa masuala ya afya wameweza kuibainisha hilo. Ambapo wanasema ulaji wa nyama, hasa nyama nyekundu una athari kiafya endapo utakuwa una kula mara kwa mara. Mfano wa nyama nyekundu ni nyama ya ng'ombe ambayo ndiyo huliwa zaidi kwa hapa Tanzania.

Japo kwa takwimu za hivi karibuni zimeonyesha ya kwamba Tanzania ni nchi ya mwisho kwa ulaji wa nyama kwa upande wa Afrika Mashariki. lakini takwimu hizo haziufuti ukweli juu ya athari zitokanazo na ulaji wa nyama nyekundu.

Zifuatazo ndizo athari za ulaji wa nyama nyekundu :
Athari za ulaji wa nyama nyekundu zipo nyingi sana ila kwa leo naomba nieleze chache.

Athari hizo ni:
  • Ulaji wa nyama nyekundu huathiri kwa kiwango kikubwa katika joint za mwili wa binadamu. 
  • Athari hizi hupelekea ugonjwa wa kuumwa kwa mwili hususani upande wa miguu.  
  • Na ndomaana tumezidi kuona ongezeko la wagonjwa wengi  ambao wanalalamika kwamba miguu inawauma.


Lakini pia ulaji wa nyama nyekundu husababisha ugonjwa wa saratani ya matiti kwa kina mama. Lakini katika upande wa kina baba ulaji wa nyama nyekundu kwa wingi umekuwa chanzo kikubwa cha kupunguza kwa nguvu za kiume kwa kiwango kikubwa.

Hivyo watalamu wa afya wanazidi kutusisistiza ya kwamba tusipende kula nyama nyekundu kwa wingi ili kuepukana na madhara hayo.  Lakini pia tunashauriwa  tusile nyama nyekundu zaidi ya mara tatu kwa wiki.