HATIMAYE MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA LINDI AACHIWA KWA DHAMANA YA SHILINGI MILIONI MBILI
Mnamo january 18 mwaka huu mahakama ya mkoa wa Lindi ilimtia hatiani mwenyeki wa CHADEMA mkoa wa Lindi Suleiman Mathew pamoja na katibu wa chama hicho tawi la Nyamangala Lindi Ismail Kapulila kwa kosa la kufanya mkusanyiko usio halali.
Hata hivyo baada jaji aliyekuwa akisikiliza rufaa hiyo Lameck Mikael kupitia maombi ya watuhumiwa aliona hakuna kipingamizi chochote cha kuwanyima dhamana, hata hivyo watuhumiwa wakiongozwa na wakili wao Deusdediti Kamalamo anazungumza haya nje ya mahakama.
Kesi hiyo ambayo ilionyesha kuvuta hisia za wafuasi wa CHADEMA kutoka mkoa wa Mtwara na Lindi huku wakiongozwa na katibu mkuu taifa wa chama hicho Dr Joseph Mashinji anazungumza haya nje ya mahakama.
Hata hivyo watuhumiwa wanaomba kesi ya msingi ya rufaa no 11 ya mwaka 2017 wanapinga kutiwa kwao hatiani na kuiomba mahakama kuondoa shauri hilo.
Watuhumiwa wanatakiwa kuripoti mahakamani kila juma la kwanza la mwezi, na kesi ya msingi itatajwa tarehe 3-5-2017.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi