FAIDA ZA MAJANI YA MPERA



Mapera ni matunda ya msimu yenye wingi wa vitamini A na C, madini ya potasiam. Licha ya watu wengi kulifahamu tunda hili wengi wao hawafahamu ya kwamba hata majani yake yana faida sana,  hasa faida za kiafya. Leo naomba tuangalie faida za majani ya mpera katika kutibu afya zetu.

Zifuatazo ndizo faida za majani ya mpera.

Unachotakiwa kufanya : chemsha maji ya moto kisha chukua majani ya mpera changanya kwenye maji ya moto kwa muda wa dakika kumi na tano, kisha yaache maji hayo yapoe. Yakisha poa chuja vizuri kwa ajili ya matumizi.

Ambapo baada ya kupata maji hayo,  maji hayo husaidia kutibu magonjwa yafutayo:
  • Husaidia kwa kiwango kikubwa kudhibiti vijidudu vya magonjwa mwilini na hasa kuzuia magonjwa ya kuharisha na kipindupindu.
  • Husaidia kutibu  mchafuko wa tumbo na pia inasaidia kukabili madhara yaletwayo na chakula chenye sumu.
  • Maji hayo hutibu kukooa na kupumua kwa tabu.
  • Upatapo uvimbe wa fizi na maumivu mdomoni kama jino kuuma, tafuna majani ya mpera kwani ni tiba tosha.


Na haya ndo matumizi ya majani ya mpera ambayo huhitaji kuchanganya na maji.

1. Husaidia kutibu kidonda katika mwili.

Unachotakiwa kufanya ni:

Ponda majani ya mpera na kuweka sehemu ya kidonda au iliyoathirika ila kuondokana  maambukizi na mambukizi mengine yatokanayo na bakteria.

2. Unapoumwa na wadudu majani yalipondwa ni tiba sahihi.

3. Majani ya mpera yana saidia kupigana na mba na chunusi kutokana na wingi wake wa vitamini C.

Mpaka kufikia hapo hatuna la ziada, tukutane siku nyingine hapa hapa Muungwana Blog.