YANGA YAFUNIKWA NA SIMBA NJE YA UWANJA
Gazeti hili lilishuhudia sehemu mbalimbali mashabiki wa Simba wakicheza na kufurahi kana kwamba walikuwa na uhakika wa ushindi kuliko wenzao wa Yanga.
Katika matawi mbalimbali, mashabiki wa Simba walionekana kuchangamka zaidi kuliko watani zao, Yanga na hivyo kuonyesha kuwa Wekundu wa Msimbazi walijiamini zaidi katika mchezo wa jana.
Shabiki wa Yanga aliyejitambulisha kwa jina la Ally Shabani alisemamapema jana kuwa anawaangalia tu Simba jinsi wanavyofanya
amshaamsha lakini jioni wasizimie wote kutokana na kipigo watakachowapa.
Shabiki wa Simba, Mohammed Ally alijitapa kuwa wako vizuri dhidi ya Yanga, hivyo wangewapiga nyingi na alifanikiwa katika utabiri kwani Wekundu wa Msimbazi walishinda mabao 2-1
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi