Habari zinasema mlipuko huo ulilenga hoteli moja katika maeneo jirani na mji wa Lahore.
Shambulizi hilo limefanyika wakati ghasia zinazohusishwa na makundi la IS na Taliban zimekuwa zikiongezeka nchini Pakistan, ambapo wiki kadhaa zilizopita takriban watu 130 waliuawa nchini humo katika ghasia.
