MZEE WA MIAKA 68 JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA


MZEE mwenye umri wa miaka 68 ametupwa jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kubaka mtoto mwenye ulemavu wa akili.

Mzee huyo, Nadhan Kifaru alitiwa hatiani na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma.

Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha mashitaka wa Polisi, Godwin Ikema kuwa mtuhumiwa alimbaka binti huyo mwenye umri wa miaka 13, Desemba 9, 2016 katika kijiji cha Makutupa wilaya ya Mpwapwa , Dodoma Kesi hiyo ya jinai namba 123 ya mwaka 2016 ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya, Paschal Mayumba.

Alipopewa nafasi ya kujitetea mzee huyo alisema yeye kutokana na umri wake wa miaka 68 hana nguvu tena za kushiriki tendo la ndoa kwa hiyo hawezi kubaka na amefikishwa mahakamani kwa chuki za wanakijiji.

Hata hivyo, hakimu Mayumba alimueleza kuwa mahakama hiyo imetia hatiani na kumtaka ajitetee ili mahakama isimpe adhabu kali.

Mshitakiwa huyo aliiomba mahakama impunguzie adhabu kutokana yeye kuwa mzee wa miaka 68 na kwamba anakabiliwa na ugonjwa wa pumu ambao hawezi kukaa gerezani.

Akimsomea hukumu hiyo hakimu Mayumba alisema kutokana na mahakama kumuona na hatia pamoja na kuzingatia utetezi wake inampeleka jela miaka 30.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.