MWANAUME ALIYEMUOA MAMA YAKE AMUACHA WAKATI WA FUNGATE


Mwanamume aliyemuoa mamake amuacha wakati wa FUNGATE (PICHA)

- Mwanamume kutoka Zimbabwe aliyemuoa mamake na kumpa talaka baada ya kutembelea kanisa moja Afrika Kusini

- Amedai kuwa mchungaji mmoja kutoka Afrika Kusini alimwondolea uchawi aliowekewa na mamake ili afanye tendo hilo

- Mama huyo hajasema chochote kuhusiana na kisa hicho

Kulingana na tovuti ya Zambian Observer, mwanamume mmoja kutoka Zimbabwe alishtua watumiaji wa mitandao ya kijamii alipoamua kuoa mamake.

Lakini wawili hao walitalakiana baada ya mwanamume huyo kusema kuwa aligundua kuwa mamake alitumia uchawi na kumfanya kutekeleza jambo kama hilo.

Aligundua hilo alipomtembelea mchungaji mmoja kutoka Afrika Kusini kwa jina Pastor Mboro ambaye alimwombea na kufungua macho yake.

Walioshuhudia kisa hicho walieleza kuwa mwanamume huyo alianguka chini wakati wa maombi na akaanza kutapika, hali iliyomvutua mchungaji huyo kwake. Alipoanza kumwombea, uchawi huo ulitoka, ambapo alifunguka macho.

Farai kutoka Zimbabwe alisema: “Mwanamke huyu ni mbaya sana, alikuwa ameniroga kwa miaka hii yote. Cha kuzidisha ni kuwa alisisitiza nile nyumbani kila siku!”

Kulingana naye, alifikiria alikuwa anampenda lakini hakujua kuwa mamake alikuwa anamwekea ‘juju’ ndani ya chakula ili aendelee kumtumia vibaya.

“Ukweli, kukiwa na wanawake wa umri mdogo na warembo itakuwa vipi nimuoe mwanamke mzee kama mamangu. Nimebadilisha nambari yangu ni sitaki kumwona tena,” Farai alisema.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.