MBOWE ANAPITIA TANURU LA WENZAKE



Sakata la kukamatwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe mwanzoni mwa wiki hii na kupekuliwa nyumbani kwake kujua kama anajihusisha na dawa za kulevya, ni sehemu ya matukio yanayowakumba viongozi wakuu wa vyama vya upinzani barani Afrika.
Kufanana kwa mazingira ya wapinzani kukamatwa yameelezwa na Profesa wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha (RUCU), Gaudence Mpangala kuwa na uhusiano na ufifishaji wa demokrasia ya vyama vingi katika nchi nyingi za Afrika.

“Ingekuwa ni makosa ya kawaida wasingekuwa wanalengwa viongozi wa vyama vya upinzani vyenye nguvu tu. Mfano Tanzania kuna vyama zaidi ya 10, lakini vinavyosumbuliwa viwili tu (Chadema, CUF) na huwezi kusikia kwa vingine,” alisema.

Profesa Benson Bana wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaa (UDSM) alisema suala hilo linastahili uchambuzi wa kina kwa kuwa lina sura mbili; wanasiasa kutumia upinzani kufanya makosa ya makusudi ili waendelee kutengeneza umaarufu, au vyama tawala kuwaonea ili kufifisha umaarufu wao.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.