MAMBO 10 MUHIMU ANAYOTAKIWA KUFANYA BABA KWA MTOTO WAKE WA KIKE



Jamii imemuachia mama kwenye malezi ya watoto, huku baba akiwa mtafutaji tu. Yaani mlipa bills. Lakini yapo mambo  muhimu sana ambayo baba anapaswa kushiriki kwenye malezi ya watoto mbali na kusaidia kipesa. Tafiti zinaonyesha binti aliyelelewa kwa karibu sana na baba yake, huwa ni binti mzuri katika mambo mengi. Yafuatayo ni baadhi ya mambo baba anapaswa kufanya moja kwa moja kwa binti yake.

1.Mjengee Kujiamini.
Baba awe mtu wa kwanza anayemwambia binti yake anampenda, tena mara kwa mara. Hakikisha
ni neno au nikitu anachojua kwa hakika kuwa baba ananipenda. Mpe muda wako, ikiwezekana pata muda wakutoka naye mkiwa wawili ili kujua anachowaza na kumjenga. Mtie moyo kwa kile anachokipenda, hata kama hajakimudu, lakin wewe ndiwe uwe wa kwanza kuwa upande wake na kuhakikisha anakimudu kwa kumtafutia walimu watakao weza kumfundisha. Kama ni mziki, basi hakikisha anaona juhudi zako za kumtafutia walimu wakumfundisha kuimba, huku ukiwepo kumtia moyo.

2. Pata Muda wa Kuomba Naye na Umuombee.
Hili ni jukumu la baba kwa asilimia kubwa sana. 
Omba pamoja na binti yako, mwambie pia huwa unamuombea unapokuwa peke yako. Utamjengea mahusiano mazuri sana na Mungu hata usipokuwepo.


3.Mpende na Kumuheshimu Mama Yake.
Waonyeshe wanao uthamani wa mwanamke. Sio
kumtukana mama yao au kubishana na kupigana mbele yao. Lazima waone uthamani unaoweka mbele ya mama yao. Yale unayotaka binti yako akafanyiwe, ndiyo aone unavyomfanyia mama yao.



4. Uwepo Wako kwenye Maisha yao.
Jitahidi kuwepo kwenye mlo nyumbani, au weka 
utaratibu wa aidha kila siku chakula cha usiku wanajua baba atakula nao au siku za Weekend. Kama ni mtoto anayefanya michezo fulani shuleni au baada ya shule, uwepo wa baba unachangia sana maendeleo bora ya mtoto. Jaribu kuhudhuria, tena hata yeye ajue kuwa uliacha kitu cha muhimu sana, kama kazi, au kuomba ruhusa kazini ili uwepo pale, kushuhudia anachofanya. Itamuongezea umakini.

5. Weka Mipaka Isiyobadilika Badilika.
Lazima mjengee mtoto na kumfundisha vitu anavyoweza kufanya na ambavyo haruhusiwi kufanya. Tena na adhabu isiyobadilika kwa yeye kulia sana atakapofanya alichokataliwa kufanya. Yaani atakapovunja sheria ulizomuwekea. Lazima kuwa makini katika hili kama unataka kulea mtoto mwenye maadili. Endapo akijua huna msimamo katika sheria zako, anaweza kuvunja na akawa salama, hawezi kuheshimu masharti yako na atakusumbua. Lazima ajue adhabu ya kila kosa na uitekeleze kwa upendo, ukiwa umetulia sio na hasira.

6. Muonyeshe Uthamani wake.
Baba ni mtu wa muhimu sana anayeweza kujenga uthamani wa mtoto. Mueleze jinsi alivyoumbwa
wa tofauti. Tena kama hufahamu vipaji vyake, pata muda wa kugundua vipaji vyake na wewe uwe mstari wa mbele kumsifia na kumtia moyo. Muonyeshe uzuri wake wa ajabu Mungu alioweka ndani yake, jinsi alivyoubwa kwa ukamilifu na vyote anavyohitaji, mwambie Mungu aliviweka tayari ndani yake. MWAMBIE YEYE NI MKAMILIFU.

7.Mwambie Jinsi Unavyojivunia Yeye.
Lazima binti yako ajue unajivunia vile alivyo, kile atakachokuwa. Lakini hakikisha unamfahamu vizuri, ili kukuza kweli jambo jema ndani yake.

8. Pata Maongezi Naye Ya Mara Kwa Mara.
Ukiwa umetulia, huna haraka na mawazo yake aone yako kwake, ongea na binti yako. Sio lazima yakawa mambo yakuonya kila wakati. Msikilize na stori zake za shule, marafiki zae, walimu, na ujue nini kimetokea kwake siku hiyo.

 Nini amefurahia na nini hajafurahia. Usiwe busy sana ukasahau muda na watoto.



9.Romance Her!
Tafuta kujua her Love Launguage, kisha umfanyie binti yako.Wengine hupenda uwe nao tu karibu 
wakati wakiendelea kufanya shuguli zao,wengine wanapenda kusikia ukimwambia nakupendawengine wanafurahia ukimkumbatia mara kwa mara na hata kupata busu la dady,wengine wanapenda kucheza pamoja. Jaribu kumjua binti yako kile anachopenda. Her Love Language, kisha mfanyie wewe kabla hajaja kudaganywa na mtu wa nje.

10. Kuwa BFF wake wa kwanza.
Hakikisha unaweka mahusiano mazuri na binti yako, ambayo atakufanya wewe ndio kimbilio 
 lake. Huku ukiweka mipaka, lakini hakikisha mbali na salamu anayokupa, kuwe kuna maongezi ya ziada kati yenu. Na hii itatokana na aina ya mazungumzo mnayokuwa nayo mara kwa mara, jinsi unavyomuonya pale anapokosea.
 Usimfanye mtoto kuwa adui hata kama ana mapungufu yake. Jua jinsi yakumsaidia sio kumuadhibu. Kwani unachotaka ni awe mtoto mzuri, sio kupunguza hasira zako kwako. Mfanye binti yako kuwa rafiki yako wa karibu.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.