MAKONDA AKATAA KUZUNGUMZIA SUALA KUGUSHI VYETI


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Dar es Salaam. Licha ya kuandamwa na tuhuma za kughushi vyeti, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hawezi kuzungumzia suala hilo kwani majibu yake yapo mtandaoni sakata lilipoanzia.

Makonda amesema hayo leo (Ijumaa) alipoulizwa swali na wanahabari kuhusu uhakika wa taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa alinunua vyeti na kutumia jina lisilo lake.

"Maswali ya mitandaoni yanaishia mitandaoni siko hapa kupoteza focus (mwelekeo).Ukiona maneno mengi yanaibuka kwenye ishu ya dawa za kulevya ndiyo ujue vita imefika penyewe,"amesema Makonda.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.