KESI YA WEMA SEPETU KUTAJWA TENA MARCH 15, BAADA YA UPELELEZI KUTOKUKAMILIKA
Wema ambaye ni Miss Tanzania 2006, anakabiliwa na kosa la kukutwa na bangi katika upekuzi uliofanywa na polisi nyumbani kwake Februari 4, mwaka huu maeneo ya Ununio jijini Dar es Salaam.
Kesi hiyo ilikuja leo kwa ajili ya kutajwa ambapo Wakili wa Serikali Nasoro Katuga alidai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo Hakimu Mkazi Thomas Simba aliahirisha shauri hilo hadi Machi 15.
Msanii huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 9, mwaka huu ambapo aliachiwa baada ya kupata dhamana ya Sh milioni tano.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi