Waandamanaji wanaompinga Trump wavunja vioo vya maduka, Binti wa Bondia Mohamed Ali naye yumo




Maryum Ali, bintiye mchezaji ndondi wa zamani Muhammad Ali, ni miongoni mwa watu wanaofanya maandamano ya kupinga urais wa Donald Trump. Maryum Ali atajiunga na maandamano ya wanawake. 

Kesho Jumamosi kunatarajiwa maandamano ya kupinga utawala wake. Hata hivyo wakati shughuli za uapishwaji wa Kiongozi huyo ukiendelea

Hali ya wasiwasi imetanda katika maeneo ya mji mkuu wa Marekani.

Waandamanaji waliovalia nguo nyeusi wametupa mapipa ya taka barabarani na kuvunja vioo vya madirisha ya maduka. 

Walinzi walifunga eneo moja la kuingilia baada ya kuvamiwa na waandamanaji wa Black Lives Matter. 

Waandamanaji waliimba nyimbo dhidi ya Trump na kuwazuia watu kuingia katika eneo hilo la kuapihswa kwa Trump .


Lakini wafuasi wa Trump waliwapigia kelele waandamanaji hao.