Ukaribu wa Nuh Mziwanda na Shilole wamfanya mke wa Nuh kusema hayat



Ulisikia  Soudy Brown jana January 27 2017  kupitia XXL Clouds FM iko na story kuhusu mke wa Nuh Mziwanda, Nawali aliyezungumza baada ya kudaiwa kuwa mume wake (Nuh Mziwanda) anafanya kazi kwa ukaribu sana na Shilole huku ikidaiwa kuwa Nawali amekuta baadhi ya ushahidi wa meseji zinazoashiri
a wako mapenzini.

Soudy Brown amezungumza na mke wa Nuh Mziwanda aliyezungumza yafuatayo……>>> ‘Nilishawahi kuona chat zake na yeye whatsup nikamuuliza akaniambia ni mambo ya show na mimi nikaona kwa nini tugombane’

‘Mimi Nawali nitabaki kuwa Nawali yule atabaki kuwa yule, halafu yule kamuona hamfai ndio maana hakumuoa ila kaona namfaa akaamua kunioa, yule ni mfamaji kwa hiyo aishi kutapatapa, yule ana watoto na familia yake ilibidi atulie na watoto wake, watoto wake wanahitaji baba pale sio kila siku watoto wanaona anabadilisha Wanaume’