Tundu Lisu asema, CHADEMA itakata rufaa kupinga hukumu ya Lijuakali kwenda jela miezi sita

Image result for tundu lissu
Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amesema kuwa chama hicho kitakata rufaa dhidi ya hukumu ya kwenda jela miezi sita ya Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mheshimiwa Peter Lijualikali wa CHADEMA, iliyotolewa jana na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero,mkoani Morogoro. Tundu Lissu amekiambia kituo cha Radio cha EFM 93.7DSM kwamba, hukumu hiyo ni mwendelezo wa dhuluma dhidi ya wapinzani nchini. Amesema CHADEMA, pia watamwekea dhamana mbunge huyo ya kuwa nje wakati rufaa ikishughulikiwa.