Simba yapigwa 1-0 na Azam ligi kuu



Mshambuliaji matata anaefahamika kwa sifa kuu ya urefu, nguvu na jicho la kuliona goli vizuri, John Bocco kutoka Azam FC leo ameisaidia timu yake ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba Sport Club katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

John Bocco katika dakika ya 70 ya mchezo aliipatia timu yake ushindi wa bao moja ambalo lilidumu ndani ya dakika tisini pasipo Simba kuweza kufua dafu na kuisaidia timu yake kupata point tatu muhimu. Hii ni mara ya pili kwa mwaka huu Simba kupokea kichapo kutoka kwa Azam Fc



Mpka sasa Simba bado ipo kileleni mwa ligi ikiwa na pointi 45, ikifuatiwa na Yanga mwenye pointi 43 ambayo kesho itashuka dimbani kuvaana na Mwadui Fc.