Raisi Magufuli afungua viwanda viwili mkoani Shinyanga

 Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli leo katika ziara yake mkoani Shinyanga amefungua viwanda viwili vya uzalishaji bidhaa. Viwanda hivyo ni FRESHO COMPANY LIMITED kinachomilikiwa na Fred Shoo wa hapa hapa Shinyanga. Kiwanda hicho kinazalisha bidhaa mbalimbali lakini leo mheshimiwa raisi amejionea uzalishaji wa mifuko ya sandarusi. 

Kiwanda cha pili ni  ni kiwanda cha JAMBO FOOD PRODUCT  kinachomilikiwa na mheshimiwa Salum Mbuzi, mbunge wa Meatu. Kiwanda hicho kinazalisha vyakula na vinywaji mbalimbali.

Akitoa hotuba yake, mheshimiwa raisi, amefurahishwa sana na juhudi zinazofanywa na wawekezaji wa ndani na kusema kuwa hawa ndio wanatimiza sera alizokuwa akizinadi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015 na akasema serikali iko pamoja nao. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akikata utepe kuashiria kufungua rasmi Kiwanda cha kutengeneza vinywaji cha Jambo food product mara bada ya kukizindua mkoani Shinyanga. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza vinywaji cha Jambo food product  Salum Hamis Mbuzi mara bada ya kukizindua mkoani Shinyanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akimsikiliza mmiliki wa wa kiwanda hicho cha Fresho,  Fred Shoo kuhusu malighafi ya kutengenezea mifuko ya Sandarusi. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiangalia moja ya hatua ya utengenezaaji wa mifuko ya Sandarusi katika kiwanda hicho cha Fresho mkoani Shinyanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiangalia moja ya hatua ya utengenezaaji wa mifuko ya Sandarusi katika kiwanda hicho cha Fresho mkoani Shinyanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiangalia moja ya hatua ya utengenezaaji wa mifuko ya Sandarusi katika kiwanda hicho cha Fresho mkoani Shinyanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwa amechuchumaa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa Kiwanda hicho cha Kutengeneza mifuko ya Sandarusi mkoani Shinyanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwagawia vinywaji viongozi mbalimbali wa dini mara baada ya kuzindua kiwanda hicho mkoani Shinyanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwagawia vinywaji kikundi cha ngoma za asili cha mkoani Shinyanga mara baada ya kuzindua kiwanda hicho cha Vinywaji mkoani Shinyanga. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwasalimia kwa kuwapungia mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora.