Mkazi huyo wa kijiji cha Matyazo Madua Saidi amekamatwa baada ya kuwepo kwa taarifa juu yake kuhusika na biashara ya bangi, ambapo mara baada ya kukamatwa mwenyekiti wa kijiji cha Matyazo Patrich Kezron pamoja na wananchi wameitaka serikali kuendesha msako vijijini kutokana na kushamiri kwa kilimo cha bangi ambacho kimekuwa kikiharibu afya za wananchi na kuzorotesha uchumi maelewano katika familia na jamii.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma kamishna msadizi mwandamizi wa polisi Ferdinand Mtui amesema mtuhumiwa huyo ambaye atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika amelima bangi hiyo pamoja na mazao mengine ili isitambulike kirahisi na kwamba msako mkali unaendelea mashambani ili kuwasaka wakulima wanaolima bangi.
