Mtoto mchanga aokotwa dampo akiwa amekufa



Pamoja na jitihada za serikali na watetezi wa haki za binadamu pamoja na haki za mtoto kupiga vita vitendo vya ukatili dhidi ya watoto bado vitendo hivyo vinaendelezwa na baadhi ya watu ambapo mtoto mchanga amekutwa akiwa amewekwa katika mfuko wa Rambo na kutupwa katika dampo la takangumu lililopo kata ya kanyenye katika manispaa ya Tabora.

Wakizungumza baadhi ya majirani wa eneo hilo wameeleza namna walivyostushwa na kitendo hicho cha kinyama baada ya kukuta mtoto mchanga akiwa ametupwa kwenye dampo la uchafu huku akiwa tayari amepoteza maisha.


Kamanda wa polisi mkoa wa TABORA ACP KHAMIS SULEIMAN amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi unaendelea ili kumbaini aliyehusika.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.