Mtoto amuua baba yake Wakati wa mkesha wa mwaka mpya
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Teonasi Malindisa mwenye umri wa miaka 68 ameuawa na mwanae kwa kukatwa na shoka kichwani usiku wa mkesha wa mwaka mpya nyumbani kwake mtaa wa Namanyigu kata ya Mshangano manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Tukio hilo limetokea usiku wa mkesha wa mwaka mpya mtuhumiwa Patrick Malindisa mwenye umri wa miaka 31 anadaiwa kumpiga baba yake kichwani kwa kutumia shoka au kitu chenye ncha kali na kusababisha kifo chake,ndugu wa marehemu wamesema kuwa baada ya mtoto kumua baba yake usiku huo alimweka ndani mpaka januari mosi saa mbili usiku alipokwenda kutoa taarifa kwa ndugu zake wakati huo alikuwa amechimba kaburi kwenye chumba kimoja kisichotumika kwa nia ya kutaka kumzika.
Marehemu alikuwa anaishi yeye na mwanae hawakuwa na Mke, majirani wamesema kuwa wote wawili walikuwa na matukio ya kuwashambulia watu kwa mapanga waliokuwa wanapita njia nyakati za usiku na kwamba hawakuwa na ushirikiano na majirani hivyo hata angezikwa humo ndani asingefahamu mtu yeyote.
Kamanda wa polisi mko wa Ruvuma ACP Zubery Mwombeji amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na wanamshikilia mtuhumiwa Patrick Malindisa kwa mahojiano Zaidi.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi