Ametoa kilio chake mbele Mwenyekiti wa wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Geita Herman Kapufi baada ya kwenda kumtembelea kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo alikolazwa kwa matibabu.
Tukio hilo la kusikitisha la kupigwa vibaya na kuumizwa sehemu za siri limetokea talehe 19 mwezi huu majira ya saa saba usiku kwenye Mgodi wa RZ unaomilikiwa na wachina katika kata ya Nyarugusu.
Akizugumza kwa shinda mbele ya mwenyekiti huyo huku akiwa amewekewa mpira sehemu zake za siri amesema kuwa tukio hilo lilitokea wakati akiwa na wenzake wawili wakipakia mawe yenye dhahabu ndani ya mifuko ya sandarusi na hapa anaeleza ilivyokuwa.
Sylvester amendelea kusema kuwa pamoja na kutendewa unyama huo na mchina huyo alikwenda katika kituo cha kidogo cha polisi Nyarugusu na kupewa PF3 lakini cha kushangaza alinyanganywa mda mfupi na askari ambaye akumfaamu mara moja kwa madai ya kuwa atakuja kuchukua kesho yake.
Mganga wa zamu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo Elias Hambohambo amekili kumpokea Mgojwa huyo na kwamba hali yake inaendelea vizuri huku Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama akisema kitendo kilichofanyika ni cha kinyama na kuahidi kuchuka hatua juu ya mchina huyo.
Channel Teni imelazimika kufika ndani ya mgodi huo na kufanikiwa kumpata Msemaji wa kampuni Frances Kiganga na majibu yake yalikuwa ni haya huku jitihada za kumpata kamanda wa polisi zikiwa hazikuzaa matunda kutokana na kuwa nje kikazi.
Ikumbukwe kuwa hili ni Tukio la pili kutokea ambapo Julai 6 mwaka jana Masanja Shilomero 25 mkazi wa kijiji cha Nyamitondo alipigwa na mwajiri wake ambaye ni mchina Myo baada ya kuomba kuogezewa mshahara.
