Madakitari watatu jijini Mwanza washikiliwa na jeshi la Polisi



Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza, limewatia mbaroni Madaktari watatu wa Hospitali ya Uhuru iliyopo wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, kwa tuhuma ya wizi wa fedha pamoja na kugushi baadhi ya nyaraka za Hospitali hiyo.

Akizungumza na Channel Ten Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi, amesema Jeshi hilo limelazimika kuwatia mbaroni Madaktari hao, ili kufanya uchunguzi ya tuhuma zinazowakabili, zikiwemo za kujipatia fedha kutoka kwa wagonjwa.

Awali akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Dk. Derick Nyasebwa, amesema kuwa Dk. Peter Kibunto siyo mfanyakazi tena wa Hospitali hiyo, kutokana na tuhuma za kujihusisha na vitendo hivyo.


Kwa upande wake mratibu wa vituo vya Afya binafsi na sekta za Umma, wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza Nyanganyi phinias, amesema kutokana na tuhuma hizo wamelazimika kuifungia Zahanati ya KB.