Lowasa asema njia ya Ikulu 2020 nyeupe



Kahama. Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema njia ni  nyeupe kwa Chadema kuingia Ikulu katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020.

“Kuweni watulivu  na mwaka 2020 mjitokeze kupiga kura na kama nitakuwa  hai nitakuwa mgombea tena wa urais kupitia muungano wa vyama vya upinzani,” alisema.

Akizungumza nyumbani kwa kada wa Chadema, James Lembeli katika kijiji cha  Mseki, Kahama, Lowassa (pichani) alisema ameshindwa kuzungumza na kufanya mkutano na  wananchi wa kijiji hicho akihofia kukamatwa na polisi kama alivyokamatwa Geita na kuwataka wawe wavumilivu hadi uchaguzi wa mwaka 2020.


Kadhalika, Lowassa aliwataka vijana wasikubali kuibiwa kura kwa madai uchaguzi uliopita hawakutendewa haki na ndio maana walikosa ushindi.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.