Jengo la kanisa la KKKT SHINYANGA laezuliwa na mvua iliyoambatana na upepo


Katika hali isiyo ya kawaida, jengo la kuabudia la Kanisa La Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Ebeneezer mtaa wa Konde Busongo manispaa ya Shinyanga limeezuliwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali sana.

KATIBU WA USHARIKA WA EBENEEZER KANISA KUU SHINYANGA  IBRAHIMU ALFRED LYANGA, akiwa eneo la tukio huko Busongo 

Akiongelea tukio hilo katibu wa Usharika wa Ebeneezer Kanisa Kuu Ibrahimu Alfred Lyanga, amesikitishwa na tukio kwani limewarudisha nyuma katika shughuli zao za usharika na itabidi kamati ya ujenzi ya usharika ikae na  kuona ni wapi pakuanzia na kuweza  kurudisha miundo mbinu hiyo ili watu waendelee kusali na kumcha Mungu katika nyumba ya kupendwa, hivyo kazi iliyopo kwa sasa  ni kubwa itakayowafanya waache shughuli nyingine kwa ajili ya kuweka sawa miundo mbinu hiyo. 

Mwinjirist wa mtaa wa KONDE BUSONGO Bwana Obed Masanja akitoa maelezo juu ya tukio hilo. 

 Maafa haya yameleta masikitiko makubwa kwa waumini wa kanisa hilo kwani yamewafanya warudi nyuma kwa kuanza shughuli mpya ya uezekaji . Akizungumza mwinjirist wa mtaa huo Obed Masanja amesema kuwa, pamoja na maafa hayo, kanisa litaendelea kumtangaza Yesu Kristo pande zote za dunia kwa kila namna.

‘’Hatutaacha kumtangaza Kristo pande nne za dunia, na kwa njia yoyote ile hata kama ni chini ya mti injili itapigwa tu’’


 Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi ya Usharika wa Ebeneezer kanisa kuu, Atutangile Luvanda akiwa eneo la tukio 

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ujenzi na mhandisi mstaafu Ndg. Atutangile Luvanda, amesema mvua iliyonyesha jana iliambatana na upepo mkali aina ya CYCLONIC WIND kiasi kwamba ni upepo mkali unaoweza kubeba hata mbuzi. Lakini pia ameahidi katika suala zima la kurejesha miundo mbinu hiyo, yeye kama mwenyekiti wa kamati ya ujenzi atahakikisha anasimamia kikamilifu ili kupunguza uwezekano wa maafa kama haya pale mvua zenye upepo mkali zinapotokea

Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi ya Atutangile Luvanda akiwa na Katibu wa Usharika Ibrahimu Alfred Lyanga wakiwa katika masikitiko makubwa juu ya tukio hili 

Mwinjirist Obed Masanja akielezea jambo flani kwa baadhi ya washarika waliofika eneo la tukio


Baadhi ya wazee wa kanisa waliofika kujionea maafa yaliyotokea katika kanisa lao

Baadhi ya washarika wakiendelea kushangaa kwa kilichotokea

Hivi ndivyo bati zilivyoezuliwa na kutupwa mbali 

Hapa ni pembeni ya kanisa

Baadhi ya bati zilizoezuliwa na upepo lakini baadae kuokotwa na kurudishwa ndani na washarika waliowahi asubuhi na mapema 

Humu ndio ndani ya kanisa 

Kanisa likiwa limebaki wazi baada ya kuezuliwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali. 

Watu hawaamini kilichotokea 

Baadhi ya washarika wa Ebeneezer Kanisa Kuu wamesononeshwa na hali hiyo lakini wakajipa moyo kwani kazi hii ni ya Mungu mwenyewe na yeye ndiye aliyeianzisha hivyo yeye mwenyewe ataparekebisha palipobomoka ili kazi yake iendelee mbele.

Mvua hiyo iliyonyesha ndani ya dakika 10 ,ikiambatana na upepo mkali imesababisha maafa makubwa kwa baadhi ya wakazi wa manispaa ya Shinyanga hususan kata za Kitangili, Chamaguha na Ushirika kwani nyumba zilizoezuliwa na kubomoka ni nyingi. 

PICHA ZOTE - ISAAC LUHENDE MASENGWA