Mlonge ni mti ambao una asili ya Uhindi, lakini kwa
sasa mti huu hupandwa kanda za tropiki.
Karibu kila sehemu ya mti huu ni tiba yaani kuanzia
mbegu zake, magome, majani pamoja na mizizi.
Hapa leo nitaanza kukwambia kuhusu mbegu za mti wa
mlonge zinavyoweza kutibu magonjwa mbalimbali kama ifuatavyo:
Magonjwa ambayo hutibiwa na mbegu za mti wa mlonge
ni pamoja na kuweka sawa shinikizo la damu, baridi yabisi na uvimbe wa magoti.
Mbegu hizo pia husaidia kutibu kifua kikuu, pumu
pamoja na matezi.
Aidha, mbegu za mlonge pia zinauwezo mkubwa wa
kukabiliana na saratani, kisukari, kukosa usingizi pamoja na magonjwa ya zinaa.
Mbali na hayo, mbegu za mlonge pia ni muhimu katika
kukabiliana na vidonda vya tumbo, homa ya matumboni, malaria sugu na maumivu ya
mwili, huku mafuta yake yakiwa ni dawa nzurikwa kuchua maumivu ya mwili.
Nitaendelea kukuletea mambo mbalimbali kuhusu
mlonge, ambapo kesho nitakuletea faida za kutumia majani ya mti huu wa mlonge.
