Chemical: Wengi wanajitokeza kunitafutia mwanaume

Wema Sepetu akiwa na Chemical

Rapa wa kike bongo Chemical ambaye siku za karibuni aliweka wazi kuwa mpaka sasa bado hajapoteza usichana wake amefunguka na kusema toka watu wamesikia jambo hilo kuna watu wengi wamekuwa wakijitokeza na kutaka kumtafutia mwanaume.

Akiongea kwenye kipindi cha eNEWZ Chemical alisema Wema Sepetu si kweli kama alikuwa anamtafutia mwanaume bali Wema Sepetu alikutana naye na alikuwa naye karibu sana kipindi ambacho walikuwa wanatengeneza filamu ya 'Mary Mary' ila amekiri kuwa wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakijitokeza na kutaka kumtafutia mwanaume.

"Kiukweli toka nimefanya vile napata comment nyingi sana wengine wanasema sikuwa na busara kufanya vile. Lakini nataka kuwaambia kwanza sikujitangaza ila ilitokea tu baada ya kuulizwa vitu ambavyo inawezekana siwezi kuvijibu. Lakini napenda kuwaonyesha watu tusilazimishe kwa kuwa wewe umepitia kitu fulani wote tunatakiwa kuwa tumepitia jambo hilo, mimi najua background yangu niliyotokea siku zote na focus kwenye 'Career' yangu sitaki kitu chochote kiniharibie hasa sijui mwanaume ajae kuniharibia maisha yangu" alisema Chemical

Mbali na hilo Chemical aliweka wazi juu ya watu ambao wamekuwa wakijitokeza kutaka kumtafutia mwanaume na kusema yeye hana shida hata wakimtafutia mwisho wa siku yeye lazima ampime kuona kama anamfaa au hafai.

"Wema Sepetu tumekutana kwa ajili ya movie, kuna movie tulikuwa tunashoot inaitwa 'Mary Mary' kwa hiyo kipindi kile watu walikuwa wananiona na Wema ni kipindi ambacho muda mwingi tulikuwa location. Ila akinitafutia kama dada means kwamba ataona kuwa huyo mwanaume ananifaaa siyo Wema Sepetu tu wapo watu wengi wanajitokeza kumtafutia Chemical mwanaume kwa hiyo kama wataona huyo mtu ni mtu sahihi kwangu waniletee na mimi nitamwangalia nikiona ni mtu sahihi sawa hivyo wanajitokeza wengi kunitafutia wanaume ila siyo Wema" alisema Chemical

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.