Mgeja adai CCM ni ile ile, aponda pangua pangua ya Magufuli

KADA wa zamani wa CCM na aliyewahi kuwa mwenyekiti wa chama hicho
mkoani Shinyanga ambaye kwa sasa yupo chama cha demokrasia na
maendeleo (Chadema) Khamis Mgeja amesema mabadiko yaliyofanywa na CCM hakuna jipya.


Akiongea na waandishi wa habari mkoani Tabora jana alisema mabadiko hayo
hayana jipya kwani CCM ni ile ile,watu ni wale wale na mambo yake ni
yale yale.

Alisema hayo baada ya kuombwa kutoa maoni na waandishi wa habari juu
ya mabadiko yaliyofanywa na CCM.

Mgeja alisema pamoja na madai ya CCM kuwa imefanya mabadiliko makubwa
sisi wachambuzi wa mambo ya kisiasa nchini tunawashangaa na kuwaona
kama wakijidhoofisha wenyewe bila wao kuitambua.

Aidha amewapa pole sana wanachama wa CCM na wajumbe wa NEC
waliopitisha maazimio hayo ambalo panga la mabadiliko limewapitia na
kupunguzwa wajumbe wa NEC 388 hadi 158.

Aidha alisema maazimio hayo ya mabadiliko sisi wanachama tuliokuwemo
ndani ya CCM muda mrefu baadaye kuachana nacho chama hicho tunaona
maazimio hayo ni sawa na kuku kujinyonyoa manyoya yake mwenyewe.

Alisema sababu za msingi za mabadiliko hayo hatuzioni kufuta nafasi ya
mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM na makamanda wa vijana wa CCM pia na
walezi wa kina mama lakini kubwa pamoja na panga la maumivu na
kuwapunguza wajumbe wa NEC.

Alisema hayo ni mabadiliko ni ya ajabu ambayo hayajawahi kutokea
tangia wakati wa TAA na TANU na baadaye CCM kwani mabaliko hajaonyesha
sababu za msingi kuwaondoa na imani zilikuwepo sababu za msingi za
kuwepo kwao zilizopitishwa wakati wa aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Dk
Jakaya Kikwete.

Alisema wamefutwa bila sababu mbadala na hata jumuiya zenyewe za chama
hazikushirikishwa .

Alisema tumeendelea kushangaa na kuwapa pole tulitegemea mabadiliko
makubwa haya demokrasia ndani ya chama ingetumika kushirikisha maoni
ya wanachama na jumuiya zenyewe.

Aidha hii imeonyesha ukandamizaji wa demokrasia ndani ya chama chao na kudhihirisha kuwa CCM ina wenyewe.

Aliongeza mabadiliko ni sawa na chama hicho ni cha watu wachache na
saa nyingine wengine hawajulikani kimetoa maamuzi kwa niaba ya wengi.

Alisema matatizo ya CCM au mafanikio tunaomba tuwaachie wenyewe lakini jambo kubwa watanzania walitegemea kuwa waone mabadiliko tunaenda wapi kisiasa na kiuchumi ni ujamaa au ubepari.

Aidha na hata uchumi tunaoujenga wa viwanda ni wa kijamaa au wa
kibepari lakini pia suala la katiba mpya maisha ya watanzania hasa
umasikini tatizo la njaa,tatizo la ajira ,mikopo ya wanafunzi,mikataba
mibovu ya madini na gesi na mafuta na kuwekwa wazi kwa mikataba na
haya ndiyo mambo ya msingi tulitegemea yazungumzwe na chama yenye tija na taifa.

Kuhusu uteuzi wa Humphrey Polepole Katibu wa NEC- Itikadi na Uenezi Mgeja amesema hajui wamemtoa wapi na kudai ni mwanachama mchanga wa chama hicho na labda sifa aliyonayo ni kuwahi kumtukana Edward Lowassa.

“Vijana tangu zamani ndani ya CCM kila aliyemtukana Lowassa alipewa cheo, nadhani Polepole naye amejipatia nafasi hiyo kutokana na juhudi kubwa za kumshambulia Lowassa katika uchaguzi wa mwaka jana,” alisema.

"Sisi wadau wa kisiasa nchini tumeishangaa CCM kumteua ndugu
Polepole tunashangazwa sijui wamemtoa wapi kwani katika siasa za
Tanzania ni mchanga mno tunamuona kama nyoka asiye kuwa na sumu ndani
ya CCM",aliongeza.

Aidha Mgeja amesema Polepole amejipambanua katika msimamo wa serikali tatu na bado amekubali kuwa mtumishi wa CCM, ambayo msimamo wake ni serikali mbili. Mtu huyu kukubali kuwa mtumishi wa CCM ni kusaliti watanzania kwani alikuwemo katika Tume ya Jaji Joseph Warioba na alipinga CCM kwa kuchakachua maoni ya wananchi.

Amesema Polepole hatoshi kushikilia nafasi hiyo na kwamba pengine nafasi hiyo ingemfaa Charles Mwijage, waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.